Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 2 YA 31

Mungu huinua watu wenye kuwapa wengine ujuzi na busara za maisha yanayompendeza yeye na watu. Ni baraka ya Mungu kama kila kizazi kina watu wenye hekima ya kuwahekimisha watu. Mkristo ana nafasi ya kuwa mtu wa namna hiyo, maana anayo maarifa yatokanayo na Neno la Mungu. Likikaa ndani ya Mkristo linafanya tegemeo lake liwe kwa Bwana: Matumaini yako uyaweke kwa Bwana, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe (m.19). Tuwaite watu wote kusikiliza, kusoma, kutii, kuhifadhi na kuishi kwa kufuata Neno la Kristo lililo hekima ya Mungu itoshayo. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu (1 Pet 3:15).

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana