Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 6 YA 31

Je! wewe mzazi unajisikiaje pale mtoto wako anapopuuza mafundisho au maagizo yako? Na wewe mtoto unajisikia vipi unapoacha kuyasikiliza, kuyapokea na kuyafuata malezi ya wazazi/walezi wako? Wazazi hufanya bidii ya kuwaelekeza watoto wao malezi bora. Hata wazazi wahalifu hawapendi wale wanaowalea waige tabia yao. Daima wapenda watoto wao wawe na tabia nidhamu ipendezayo. Wafurahi wazazi wako kama isemavyo amri fulani katika zile amri 10 za Mungu! Faida ya kuwatii wazazi ni ipi? Katika Efe 6:1-3 Paulo anafafanua ilivyoandikwa katika Kut 20:12, Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana