Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 5 YA 31

Historia ya ulimwengu ina msingi imara utokao kwa Mungu mwokozi. Ni mkombozi anayewalinda watu dhidi ya ukatili wa kila aina. Mungu anawataka watu wote wasikie na kufundisha Neno lake. Neno hilo linazo nguvu za kuwatengeneza watu ili wawe wema. Neno la Mungu ni mwongozo unaowaadilisha watoto na wakubwa. Kusikiliza kwa makini ni dalili ya hekima. Wajibu wa kuwafundisha watoto adabu umewekwa mikononi mwa wazazi. Watoto wanaofuata maonyo hupata baraka. Kwao kuna kesho ya milele.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana