Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 3 YA 31

Mungu anapenda wema na haki. Wema na haki ni tabia ya kimungu, na Yeye anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema (Mik 6:8)! Dhuluma haimpendezi Mungu. Yeyote adhulumuye ni adui wa Mungu. Wote wanaonyanyaswa na kunyang’anywa hali zao wasikate tamaa. Mungu yupo hajawaacha, anawatetea. Wote wasiotenda haki wana mwisho mbaya. Badala ya kudhulumu wengine, fanya kazi za halali kwa bidii. Mungu anatuita tutendeane haki. Wala tusidhulumiane ardhi, na mali nyingine. Ni wajibu wa viongozi kulinda na kutetea haki za wanyonge.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana