Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 11 YA 30

Kuhani Mkuu na watu wake waliaibishwa sana, ila jina la Yesu lilitukuzwa na watumishi wake walikuzwa. Lakini pamoja na ushindi wao mitume hawakuwa na majivuno. Bali Roho Mtakatifu aliwapa unyenyekevu na hekima. Maana kwa upande mmojawalimheshimuKuhani Mkuu kama kiongozi, yaani walikuja kwa hiari kusimama mbele ya baraza (m.26). Kwa upande mwinginehawakumtii, maana Mungu mwenyewe aliwatuma kushuhudia na kufundishawakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu(m.29). Kutoka kwao tunajifunza kwambakila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu(Rum 13:1).

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/