Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Paulo akiwa kifungoni huko Rumi ndipo alipomwandikia barua Filemoni aliyekuwa anaishi mji wa Kolosai. Upendo na imani ya Filemoni inamfariji Paulo na kuwachangamsha waamini kwa ujumla. Maana imeleta matokeo makubwa katika maisha ya Filemoni. Amefungua nyumba yake iwe mahali pa ibada za usharika, na imani yake inaendelea kumpa ujuzi wa baraka zote au kila kitu chema tulicho nacho katika Kristo. Tumshukuru Mungu kwa waumini kama Filemoni, na tumwombe Mungu atujalie kuiga imani na upendo wake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/