Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 2 YA 30

Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake(m.32). Mitume wana sababu zipi za kushuhudia ufufuo wa Yesu?1.Wenyewe walimwona baada ya kufufuka kwake, tena wakala chakula pamoja na akawatokeamuda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu(1:3).2.Yesu alimtuma Roho Mtakatifu juu yao kama alivyoahidi.Amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia(m.33). Hii ni dalili kwamba kweli ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba; kweli yu hai; kweli yu pamoja nao.3.Jambo hili limetabiriwa na manabii wa Agano la Kale ambalo kwao Wayahudi lilikuwa ni Maandiko Matakatifu (Biblia yao). Katika (m.25-28) tunasoma,Daudi ataja habari zake[Yesu], Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike. Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/