Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Kwa jina la Yesu Kristo waNazareti (m.6) Petro na Yohana wakamponya mtu aliyekuwa kiwete toka kuzaliwa (m.2), na watuwakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata(m.10). Kweli ni mwujiza, na hata siku hizi inatokea, lakini tusishangae sana. Maana ndivyo Yesu alivyoahidi akisema,Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi ... mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya(Yn 14:12-14). Kusudi la Yesu kutenda miujiza hata leo nikulithibitisha lileneno(Mk 16:20). Jambo kubwa linalotakiwa kuwa katikati ya huduma ya kanisa ni huduma ya NENO!Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali(Mdo 2:40-42).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/