Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Anania alikuwa amewaambia mitume kwamba ameuza mali, na thamani yake ameamua kutoa kwa kanisa. Ila ilipofika siku ya kuwapelekea mitume fedha hizo akaamua pamoja na mke wake wasipeleke zote. Huenda walipanga mahitaji fulani. Kwa hiyo unafiki ukawaingia, maana mbele ya kanisa walieleza kwamba ni fedha zote walizopata kwa kuuza mali. Wakasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo(m.8). Hivyo wakawa waongo. Matokeo yake yaliwatisha watu na yanatutisha sisi! Twajifunza jambo muhimu: Mungu niMtakatifu! Katika 1 Pet 1:14-17 tunasoma,Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/