Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa(m.21 na 32). Kwa macho ya kibinadamu Bwana Yesu alichelewa. Lakini Yesu alijua yote tokea mbali, ndiyo maanaakawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha(m.11). Tena ilikuwa ni hatari kwa Yesu kwenda Bethania, maanawale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe(m.8). Lakini upendo wake kwa wafiwa ulimsukuma aende, maanaalimpenda Martha na umbu lake na Lazaro(m. 5)! Martha alipoonyesha imani yake juu ya ufufuo siku ya mwisho (m. 24,Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho), Yesu alimfundisha akisema:Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi(m.25). Je, unasadiki hayo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/