Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Bwana, yeye umpendaye hawezi(m.3). Walimshirikisha Yesu matatizo yao. Nasi tufanye hivyo! Katika Flp 4:6-7 Mungu mwenyewe anatukaribisha akisema,Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Katika m.4 imeandikwa:Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni ... ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.Hulingana na ilivyoandikwa kuhusu yule kipofu tangu kuzaliwa katika 9:1-3,Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.Yesu anaposema,Ugonjwa huu si wa mauti,maana yake ni kwamba bado Lazaro ataendelea kuishi. Huu si mwisho wa maisha yake. Wakati mwingine ugonjwa ni wa mauti, yaani, mwisho wa maisha ya mtu. Tunapoomba uponyaji tuseme, "Mungu akipenda"!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/