Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Yesu alipowaambia Wayahudi kuwa yeye ndiye Kristo hawakusadiki maneno yake yenye upole na hakikisho la uzima wa milele. Mazungumzo yao yalikuwa hivi: Wayahudi walimwuliza,Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia(m.24-25). Hata ishara nyingi na kazi njema alizotenda hazikuwasaidia kumtambua Kristo wa Mungu. Kwa nini? Waling’ang’ana katika ujinga na kutofahamu kwao Neno la Mungu, basi wakamshtaki Yesu kuwa amekufuru. Walitaka kumwua tu. Lakini yeye akawaambia,Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba(m.37-38). Je, unaona si rahisi kumwamini Yesu? Fanya anavyoshauri hapo, Zingatia jinsi anavyoshuhudiwa na kazi alizozifanya!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/