Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Ni kawaida kufikiria kuwa mchungaji wa kondoo awapende kondoo wake. Lakini Yesu anatupa sifa na vigezo vya mchungaji mwema vilivyo vipya,Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo(m.11). Ni neno la ajabu! Nalo tumelipata kwa Yesu Kristo peke yake. Ndiye peke yake Mchungaji mwema. Kwa ajili ya kutupenda sisi aliutoa uhai wake ili tuokolewe kutoka katika dhambi zilizotutenga na Mungu. Ni heri kuwa kondoo wake, na Yesu anasema wazi katika m.16 kwamba anataka hivyo:Kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/