Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 10 YA 30

Paulo akimaliza mafundisho juu ya mpango wa Mungu kwa Waisraeli, amejaa sifa na shukrani! Anamtukuza Mungu kwa ajili ya njia zake za ajabu! Mungu ni mwaminifu! Kutokana na ahadi zake kwa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii, hawezi kuliacha daima taifa lake teule.Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake(m.29). Tuna bahati, sisi tuishio leo, maana twaona ahadi hizi zikitimizwa mbele ya macho yetu! Waisraeli wamepewa tena nchi yao ya ahadi (mwaka 1948), na wanazidi kurudi kwa wingi kutoka dunia nzima (ukipenda, soma Yer 23:5-8)! Bwana yu karibu!

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/