Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 12 YA 30

Hekima humpa mtu maongozi ya jinsi ya kuongea neno zuri wakati wa kufaa, na kuamua mambo yapasayo. Neno la Mungu ni mwongozo bora. Linatuongoza katika kujua jinsi ya kuwatendea wengine. Usifanye maamuzi kwa pupa. Uwe mwangalifu na matumizi ya ulimi wako, ukikumbuka ilivyoandikwa katika Yak 3:9-12:Kwa huo [ulimi] twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu. Mungu akufundishe kutenda unachokisema na kukiahidi kwa uaminifu. Neno la mwenye hekima kwa mtu msikivu ni bora kuliko pete au vito vya dhahabu safi (m.12:Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo).

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/