Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano
Mithali katika sura ya 25-29 zilikusanywa na viongozi wakati wa mfalme Hezekia, huenda kwa sababu ziliwasaidia kuwa na mwenendo mzuri katika kitala cha mfalme. Viongozi bora ni wale wanaotii sheria na maagizo ya Mungu. Watu wenye busara hawatafuti heshima ya binafsi. Hivyo, usijiinue wala kutafuta sifa za binafsi. Jifunze kujidhili, ukimpaMungunafasi akuinue. Katika Lk 14:7-11 Yesuakawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Kumbuka Yesu Kristo alivyojinyenyekeza na jinsi utii wake ulivyoleta wokovu na baraka kwa ulimwengu wote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/