Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Ukoo wa Yesu uliandikwa ili kuthibitisha kuwaYesu ni mwanadamu kweli. Kwa Wayahudi alikuwa mtu wa kawaida tu. Hata Pilato alimlinganisha na Baraba. Lakini ukoo huu ulipata baraka za Mungu zilizoyafikia mataifa yote; maana kutokana na ukoo huo, mkombozi wa dunia nzima alizaliwa. Mungu ametushirikisha baraka zake sawasawa na unabii wa Isa 7:14 usemao,Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Huthitibishwa katika Mt 1:23,Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli. Yesu ni "Imanueli", yaani "Mungu pamoja na wanadamu". Tofauti yake na sisi ni alivyochukuliwa mimba tu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu(m.18).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/