Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano
Yesu alitwaa mwili katika bikira Mariamu. Mimba yake ilitungwa kwa uwezo Roho Mtakatifu. Mwanzoni, hata Yusufu aliyekuwa mchumba wake Mariamu hakujua mpango wa Mungu. Aliazimu kumwacha kwa siri Mariamu ili kumwepusha na aibu. Yusufu alikuwa mtu wa haki, tena alimpenda Mariamu. Baada ya kujulishwa na Mungu kuwa mimba aliyokuwa nayo Mariamu ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Yusufu akamwoa Mariamu. Mtoto akaitwa Yesu, sawa na malaika alivyomwambia,Utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao(m.21). Jina linaeleza sababu ya kuzaliwa kwake, kwamba atakuwa mkombozi wa ulimwengu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/