Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Ulimwengu ulilaaniwa dhambi ilipoingia. Mauti, magonjwa na maovu ya kila aina yamesababishwa na laana hiyo. Yesu Kristo ameiondoa laana akichukua dhambi za watu wote na kufanywa laana badala yao:Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona(Isa 53:4-5). Katika Yesu kuna uponyaji, kiroho na kimwili. Uponyaji wa mwili hatuuoni sana hapa duniani. Wapo wanaoponywa kwa mwujiza hapa hapa, ila wengine watauona Mbinguni. Na wote hufa. Lakini tunaamini ufufuo wa mwili! Hapo ushindi tulio nao katika Kristo utakamilika kwetu kabisa.Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake(Flp 3:20-21)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/