Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Je! umekuja kututesa kabla ya muhula wetu(m.29)?Agano Jipya linatufundisha kwamba Shetani na malaika zake wana muda mfupi tu. Ndipo watatupwa katika ziwa la moto au jehanamu. Na huko watateswa milele. Shetani anajua haya. Kwa hiyo ana hasira kubwa (unaweza kusoma zaidi juu ya hasira yake katika Mt 25:41, Rum 16:20, Ufu 12:12 na 20:10). Kuhusu namna ya kutoa mapepo tufuate mfano wa Yesu. Linalohitajika ni neno tu! Neno la Yesu lina amri na nguvu.Akawaambia pepo, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka majini(m.32). Nguvu twapata ikiwa maisha yetu yamejaa neno la Mungu, maombi na toba
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/