Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Kwa kadiri ya imani yenu mpate(m.29).Watu waliposikia habari za Yesu, wengine walipokea kwa imani, kwa mfano yule bwana mwenye binti aliyekufa anasema katika m.18,Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.Fikiri pia juu ya huyu mwanamke mgonjwa alivyosema moyoni mwake,Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona(m.21). Yesu anamwambia,Imani yako imekuponya(m.22). Ila wengi hawakuamini, hata baadhi yaowakacheka sana(m.24). Hao vipofu wawili walimwamini Yesu. Waliona jambo ambalo wengi wenye kuona hawakuona. Walitambua kwamba Yesu ni Kristo, Mwokozi aliyeahidiwa na Mungu. Imani hii waliionyesha kwa kumwita ‘Mwana wa Daudi’ na kwa kuamini uponyaji wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/