Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Yesu anasisitiza kwamba tusishangae ikiwa hali ya maisha yetu kama wafuasi wake itafanana na hali yake mwenyewe. Maana yeye ni mwalimu, sisi ni wanafunzi, namwanafunzi hampiti mwalimu wake ... Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake(m.24-25). Yesu anajua maneno haya yanaweza kututia hofu, kwa hiyo anasisitiza mara tatu,Msiogope (m.26, 28, 31).Hata kama watu watajaribu kutulazimisha kulikana jina lake tusiogope, maana yeye atakuwa pamoja nasi papo hapo na kututia nguvu. Hata tukiuawa tutashinda tu, maana ajuaye yote na mwenye kuhukumu yuko upande wetu. Ndiye Baba yetu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/