Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Kuwa Mkristo wa kweli au kuwa mtumishi wa kanisa uliyetumwa kwa watu, mara nyingi kuna ugumu wake. Hali hii Yesu hutuambia wazi. Watu wengi hawataki kusikia ukweli, na wanataka wewe usiufuate ukweli. Giza linachukia nuru. Hapo panahitajika uvumilivu, kama Yesu anavyosema,Mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka(m.22). Katika Yn 15:18-21 anasema,Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka. Lakini Yesu pia hutupatia faraja. Katika mambo yote tuko chini ya uongozi wake. Hata tukikutana na mambo magumu sana hatutakosa kuona uwepo wake! Tena atatuwezesha kumshuhudia hata katika hali hiyo ngumu. Tafakari ahadi yake katika m.20,Si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/