Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Mmepata bure, toeni bure(m.8).Mitume walikuwa wamepata bure. Yaani hawakumlipa Yesu chochote ili awakubali wawe wafuasi wake na mitume wake. Yesu amewapokea kwa neema na amewaita kwa neema. Ni jambo moja tu lililowastahilisha: walimpokea Yesu na maneno yake. Ni watu walioitika. Basi wafanye vilevile. Wasidai chochote kwa watu watakapowahubiria Injili na kuwafanyia huduma yao ya ajabu. Watakaowakaribisha na kuyapokea maneno yao ndio wanaostahili.Nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu(m.13-14). Je, unayatoa bure uliyopokea bure?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/