Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Jina la mtoto wa pili, Lo-ruhama, latabiri kuwa Mungu hataendelea kuihurumia Israeli (Ufalme wa Kaskazini) kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, bali huruma yake itakuwepo upande wa Yuda (Ufalme wa Kusini), wakimtegemea Mungu wala si siasa:Nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa Bwana, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi(m.7). Jina la mtoto Lo-ami laonyesha Mungu kuikataa Israeli. Mungu hana ushirika na dhambi. Lakini mwanadamu hawezi kubatilisha mpango wa Mungu. Mungu atausimamisha na kuwaokoa watu wake, wakimtegemea kiongozi fulani atakayetokea. M.11 ni unabii juu ya Yesu:Wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/