Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

SIKU 5 YA 30

Kweli Mungu awapenda watu wake. Atawarudisha tena katika hali yao ya kuwa “mkewe”. Kwanza ataondoa baraka zake na kuharibu ibada za miungu (2:7, Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona. Tena Mungu anasema katika m.11-12,Nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa. Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila). Hivyo wangesikiliza tena neno lake la upendo na kuliitikia kwa imani.Angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo.Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri(2:14–15). Na Waisraeli watamwita Mungu “Ishi” (= mume wangu), wala si “Baali” (= bwana wangu). Katika Biblia, “kuposa” (m.19:Nitakuposa uwe wangu kwa milele) ni kufanya agano lenye masharti kama ndoa yenyewe, isipokuwa hawakai pamoja. Kwa kutazama ndoa ya Hosea na mkewe, maisha yako na Mwumba wako yakoje?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/