Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Njia ya wokovu si ile ya mwenye dhambi kumkimbia Bwana, bali amkimbilie kwa kutubu. Hapo Hosea anajihusisha na watu wake wanaohitaji toba; hata anawasihi sana wamrudie Bwanapamoja. Tatizo lenyewe si kwamba Waisraeli hawamjui Bwana. Wenyewe wanasemezana,Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya ... Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana(m.1-3). Lakini itikio lao ni la juujuu tu. Katika m.4 Mungu anawaambia,Fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema. Toba ya kweli haipatikani kwa njia ya sadaka, kama wanavyodhani, bali hutoka ndani ya mioyo yetu (ili kutafakari jambo hili zaidi usome Mt 9:9–13 na 12:1-7). Fikiria pia kuwa huenda neno hilibaada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua(m.2) ni sababu ya Yesu kusema atafufuka siku ya tatukama yanenayo maandiko.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/