Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Mwisho mbaya wa Efraimu (Ufalme wa Kaskazini) umelinganishwa na mwanzo mwema wa watu wa Mungu (Israeli katika 9:10 ni Waisraeliwote). Mungu aliwachagua wakiwa Misri, akawapenda sana, akataka kuwaleta katika nchi ya ahadi. Lakini kabla ya kuingia, wapendwa hawa walijiweka wakfu kwa miungu ya kigeni ili wabarikiwe nao (habari za kihistoria zipo katika Hes 24:1-5; kambi yao ya mwisho kabla ya kuingia ilikuwepo Baal–Peori). Kwa kuwa Efraimu imeshikamana na uovu huo, Mungu atawacha (m.12:Wajapolea watoto wao, mimi nitawanyang'anya watoto wao, asisalie hata mtu mmoja; naam, ole wao! Nitakapoondoka na kuwaacha), kuwafukuza na kutowapenda tena (m.15:Kwa sababu ya uovu wa matendo yao nitawafukuza watoke katika nyumba yangu; sitawapenda tena; wakuu wao wote ni waasi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/