Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Upendo wa Mungu kwa watu wake ni kama upendo wa baba kwa mwanawe. Tangu Misri Mungu amewalea kwa upendo:Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri(m.1).Lakini wameudharau na kumwacha Baba yao. Hivyo adhabu ipo. Lakini haina maana kuwa Mungu hawapendi, ila hawezi kujifanya kama haoni maovu yao. Angalia yale mapambano makali moyoni mwa Mungu yanayotokana na jinsi anavyopenda sana hao waliomwacha:Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuponya, Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja. Sitatumia ukali wa hasira yangu, sitarudi kumwangamiza Efraimu; kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji(m.8–9). Huonesha wazi lengo la ukali wa Mungu uliowahi kuwapata: Laiti kama wangemgeukia tena ili uhusiano wao wa awali wa kupendana ufanywe upya!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/