Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Israeli waliongeza madhabahu na kuabudu sana, maana walidhani baraka zilitoka hapo. Lakini walichokipanda kwa njia hiyo ndicho wanachokivuna sasa, yaani hukumu (m.4:Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba). Haitakuwa kama walipomtumikia Bwana. Hapo waliipenda kazi yao na kuvuna fadhili. Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; … uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki (m.11–12). Bali sasa wanakula matunda ya uongo wao wakivuna uovu (m.13:Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo). Katika m.8 imeandikwa kwambawataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni. Habari hii imetumika katika Agano Jipya kueleza jinsi wasioamini watakavyotaka kujificha wasipatwe na hasira ya Mungu:Nipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Fufunikeni(Lk 23:30),wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo(Ufu 6:16). Ndiomoyo wao uliogawanyika(m.2) uliowafikisha hapo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/