Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Katika mafanikio yao, Israeli hurudia makosa mawili ya zamani. Moja ni majivuno ya Efraimu:Alijitukuza katika Israeli(m.1). Lingine ni Waisraeli kutaka wawe na mfalme. Katika m.10 Mungu anawauliza,Yuko wapi sasa mfalme wako, apate kukuokoa katika miji yako yote? Na hao waamuzi wako, uliowanena hivi, Nipe mfalme na wakuu?(taz. 1 Sam 10:19). Yote ni kumkataa Mungu. Ingawa wanaweza kuona matokeo yake (m.1b:Alipokosa katika Baali, alikufa), wanazidi tu kujivuna na kusahau ni Bwana peke yake aliyewalisha mema.Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau mimi(m.6). Sasa Mungu akiwa kama simba kwao, watagundua wenyewe ni kama kondoo bila mlinzi. Sisi tunategemea kupata usalama toka kwa nani? Mfalme aletaye usalama kiroho na kimwili ni Yesu peke yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/