Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Mungu hawezi kumpenda tena mtu aliyerudi nyuma? Zingatia Bwana alivyo:Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha. Nitakuwa kama umande kwa Israeli(m.4-5a)! Kwa hiyo wanaorudi kwa Bwana, watafufuka kama ngano na kumzalia matunda mema, kama ilivyoandikwa katika m.7-8:Wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.Ndio wote wanaoitika Mungu anapotaka kuwaponya kiroho. Watakwenda katika njia yake nyoofu, lakini wote wenye moyo usio safiwataanguka ndani yakenjia hiyo (m.9) kama taifa la Israeli lilivyoangamia mwaka 772 k.K. Tunapomalizia kitabu cha Hosea, je, umepata ujumbe gani? Ona kwamba hayo yaliwapata Israeli ili kutuonya sisi wa leo pia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/