Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Kwa miaka mingi Waisraeli wamejiwekea hazina ya hatia. Wafanana na mtoto anayetakiwa azaliwe lakini hataki.Utungu wa mwanamke mwenye mimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili; maana wakati umewadia, ambao haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto(m.13). Tatizo lipo kwa mtoto mwenyewe. Hana akili. Hali hii imesababisha taifa kukaribia maangamizi. Katika upendo wake, Mungu bado anatazamia kuwakomboa watu wake, hata kama ni kupitia mauti. Maana ndiye mshindi wa mauti, kama anavyosema katika m.14,Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu(unaweza kusoma zaidi juu ya jambo hili katika 1 Kor 15:50-57). Siyo kwamba Mungu ataghairi na kuacha hukumu yake, bali katika rehema zake atawaokoa Waisraeli wakijuta na kumrudia yeye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/