Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Israeli wana jina la Bwana mdomoni lakini hawamtegemei. Mikataba yao na mataifa ya kigeni inathibitisha udanganyifu huo. Mungu anawashuhudia kwa maneno haya,Efraimu amenizinga kwa maneno ya uongo ... nao wafanya agano na Ashuru(11:12-12:1). Hivyo wanafanana na baba yao mkuu, Yakobo (tazama Mwa 25:22-26; 32:24-30 kwa habari zake za kihistoria). Wafanyabiashara wa Israeli wamekuwa matajiri kwa njia ya udhalimu na hongo. Lakini hawawezi kumhonga Mungu Mtakatifu, na watahukumiwa sawasawa na matendo yao, ingawa udanganyifu wao umewafanya wasione hayo ni maovu (m.8:Katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi). Maana wamekataa kutii wajumbe ambao Mungu aliwatuma kwao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/