Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Waisraeli wasifurahi kwa ibada za kipagani, maana ni uzinzi wa kiroho umchukizao Mungu. Mashamba, vyakula na mizabibu vitateketea. Watakaa utumwani na kutiwa unajisi.Hawatakaa katika nchi ya Bwana; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula kinajisi katika Ashuru(m.3). Kwa hiyo hawatakuwa na kitu cha kumtolea Mungu sadaka wala mahali pa kumwabudu, na nchi yao itabaki ukiwa.Hawatammiminia Bwana divai, wala hazitampendeza sadaka zao; mkate wao utakuwa kama chakula cha matanga kwao; wote watakaokila watatiwa unajisi; kwa maana mkate wao utakuwa kwa shauku zao; hautaingia katika nyumba ya Bwana(m.4). Waisraeli wadai Hosea ana wazimu na kutaka wamwue, ingawa ni mlinzi wao ambaye Mungu amewapelekea ili kuwarudisha kwa Mungu. Je, sisi tunafanya nini na ujumbe wa Mungu tunaoupata kupitia wajumbe wake?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/