Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Hosea ni muhtasari wa kuharibika kwa Israeli. Wamelivunja agano la Mungu. Wafalme wao sio chaguo la Mungu, kwa hiyo wamegeuka kuwa mzigo kwa Israeli. Hawamjali Muumba wao, bali maabudu yao ni ya kipagani.Kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu(m.4). Wamejinunulia upendo kwa nchi jirani,kwa maana wamekwea kwenda Ashuru(m.9), lakini upendo wa Mungu haununuliki kwa matoleo. Haohutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini Bwana hawakubali(m.13). Hali waliyo nayo kwa sasa inafananishwa na punda wa mwituni asiye na kiongozi. Maana tukikataa kuongozwa na Mungu, hayupo kiongozi mwingine wa kuaminika. Mwishowe watapelekwa uhamishoni.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/