Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

SIKU 11 YA 30

Taifa la Israeli litaangamia. Wenyewe wamewaua wafalme wao wanne kwa miaka michache (angalia 2 Fal 15:8ff kwa ajili ya kusoma matukio ya kihistoria). Hosea anabainisha sababu: Wanaona hali yao si nzuri, lakini hawaelewi msaada wa kweli ni kwa Bwana, maana uongo wao umewadanganya. Katika kiburi chao wanategemea siasa ya kushirikiana na Misri na Ashuru bila kuelewa kwamba wageni hao wamekula nguvu za taifa (m.9-11:Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari.Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru). Waisraeli wanakusudia hata udhalimu juu ya Mungu, ingawa anataka tu awaponye na kuwakomboa katika uharibifu ule wanaouelekea. Mwenyewe anasema katika m.13,Ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenene uongo juu yangu(unaweza pia kurudia m.1 na 14-15).

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/