Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Watu wa Mungu wapata adhabu kwa sababu ya makosa yao. Wametawaliwa na ibada za miungu. Mioyo yao imekuwa migumu kiasi cha kutotaka kurudi kwa Mungu. Dhambi ina nguvu kubwa ya kiroho. Inampofusha anayeitenda.Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui Bwana. … Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe wamtafute Bwana; lakini hawatamwona(m.4 na 6). Kiburi cha mwenye dhambi kinachangia pia asimgeukie Mungu.Kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao(m.5). Israeli wana mipango na Ashuru (m.13:Efraimu alipouona ugonjwa wake, … ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu). Hii itawaletea maafa makubwa toka kwa Mungu. Maana usalama wapatikane tu kwa kutubu na kumrudia Mungu, mchunga kondoo wao. Tunapoonywa tusiwe wakaidi, kwa sababuaonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula, wala hapati dawa(Mit 29:1).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/