Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano

Hosea anatazama moja kwa moja hali ya taifa la Israeli. Watu wamemwasi Mungu kwa njia nyingi (angalia tena m.1-2). Uovu wao umesababisha hali ya ukame katika nchi. Lakini makuhani wamefurahi.Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao,maana dhambi zikizidi sadaka za dhambi zitazidi, na hivyo itazidi faida yao kwa mambo ya mwili (m.8).Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Angalia sanasababu yakekatika m.6: Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Ni onyo kwetu tulio na huduma kanisani. Adhabu ya Mungu itakuja bila upendeleo.Kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani, yaani huyu aliyewafundisha (m.9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/