Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Ibada zipo ili tujifunze katika utulivu na utiifu, Neno la Mungu linapohubiriwa. Sababu ya mwanamke kutajwa kipekee ni katazo katika m.12:Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Neno hili linahusu yale mafundisho kanisani yaliyo ya lazima kutiiwa na washarika wote. Mwenye huduma hiyo awe muumini mwanamume mwenye karama ya Roho. Kuna sababu mbili. Moja ni jinsi Mungu alivyomwumba mwanadamu:Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye(m.13). Sababu nyingine ni jinsi anguko katika dhambi lilivyotokea:Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.(m.14). Lengo ni wokovu wetu. Ndivyo Paulo anavyokaza katika m.15, akiandika kuhusu mwanamke kwambaataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi(m.15). Utaratibu huo haumzuii mwanamke kumwomba, kumshuhudia na kumsifu Mwokozi na Bwana wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz