Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Kanisa ni familia ya Mungu, na familia yetu ya nyumbani ni kanisa dogo. Kwa hiyo kumtumikia Mungu katika usafi wa kiroho hufungamana na malezi ya familia. Hayo ni jukumu ambalo halikwepeki. Leo tunakumbushwa kuwa tuwalee watoto wetu katika imani na maadili mema ya kumjua Yesu Kristo:Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao(m.12).Tutengemuda maalumu wa kukaa na familia ili mahangaiko mengi ya kikazi yasiwe kisingizio cha kutosoma Neno la Mungu na kuomba pamoja. Ujasiri mwingi wa mtumishi hutokana na familia yake kumwunga mkono.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz