Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Je, kijana kama Timotheo anaweza kumkosoa mtu mwenye umri mkubwa? Ndiyo, anajibu Paulo, ilaumwonye kama baba(m.1)! Lakini je, neno hili linaleta maana yoyote hapa Tanzania? Si kwamba baba hana kosa? Mungu atusaidie sisi sote, vijana kwa wazee, kuelewa maana ya amri yake kuhusu kuwaheshimu baba na mama (Kut 20:12,Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako). Kanisa lina wajibu wa kuwasaidia waumini walio na hali ngumu. Lakini hao wakiwa na familia yenye uwezo, wajibu wa kuwatunza hauko tena kwa kanisa bali kwa familia. Utunzi huu wa kifamilia na imani ya kikristo haviwezi kutenganishwa, Paulo anakaza katika m.8:Mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz