Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Ndivyo Paulo alivyomwambia Timotheo katika m.20. Jambo hili la kuwakemea rasmi wanaoendelea kutenda dhambi linamfanya Paulo kutoa onyo kali sana juu ya upendeleo. Kuharakisha uamuzi au hukumu kuna hatari kubwa: Tunaweza kujikuta tunashiriki dhambi za watu wengine. Ni busara kutomkataa mtu kwa haraka, na vilevile kutompokea mtu kwa haraka kuwa mtumishi.Hawa [wanaotaka kuchaguliwa kuwa watumishi] wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia(3:10). Mtu akijaribiwa hivyo kwanza, mara nyingi itakuwa dhahiri ni wa aina gani, ama kwa njia ya dhambi zake au matendo yake yaliyo mazuri. Ndivyo Paulo anavyokumbusha katika m.24-25:Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata. Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika. Basi,ujilinde nafsi yakokwa kuepuka dhambi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz