Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Maisha ya Mkristo yana vita vya kiroho. Adui mkuu ni shetani, na mashindano ni ya imani kuhusu uzima wa milele. Timotheo amekiri imani yake mbele ya Wakristo, sasa ashikamane nayo mpaka mwisho. Katika vita hivi kuna kukimbia na kukimbilia:Wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole(m.11). Katika m.12-13 Paulo anaendelea kueleza kwamba kukimbilia huko hufungamana na kufuata mambo fulani:Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. Vilevile kukimbilia huko hufungamana na kumtazama mtu fulani, yaani Kristo Yesu:Nakuagiza ... mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato. Yesu mwenyewe ni kielelezo chetu, tena tumaini letu. Atafunuliwa kwa utukufu mkuu na Mwenye uweza ambaye peke yake hapatikani na mauti. Tumtazame Yesu, nasi tutashinda vitani!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz