Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Je,utauwa ni njia ya kupata faida? Neno la Mungu lasema hapana. Kwa nini basi, siku hizi wengi wasema ndiyo? Hata wapo wanaosema ujumbe huo ni injili! Paulo anaonesha kwamba majivuno juu ya mali uliyopewa hupofusha. Mtu aliyejivunahafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya(m.4). Kupenda fedha huleta mabaya tu. Hiyo ‘injili ya mafanikio ya kiuchumi’ siyo Injili. Biblia inasema kwambahatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu(m.7)siku ya kufa. Hata hivyo utauwa una faida kubwa. Hutupakuridhikatukiwa hapa duniani nauhakika wa kwenda kuishi milele na Yesutunapofariki dunia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz