Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Inatokea kwamba viongozi kanisani (ni maana ya “wazee” hapa)watawalao vemawanasingiziwa mambo mbalimbali yasiyo kweli, pengine na wenye umri mdogo zaidi wanaoonea madaraka yao. Tusikubali tu mashtaka haya, bali tudai mathibitisho ya mashahidi. Wewe ukiwa kiongozi, kumbuka shahidi wa kwanza ni utumishi wako mwenyewe. Hiyo imedokezwa katika m.17 Paulo anaposema:Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kiongozi akifanya kosa asaidiwe kulirekebisha, lakini kama yupo kiongozi anayeendelea kutumia vibaya madaraka yake, asihamishwe tu, bali dhambi yake ikemewe rasmi kanisani:Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope(m.20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz