Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Inaonekana kanisa lilikuwa na orodha ya wajane waliotunzwa nalo kila siku hadi kufa, na walikuwepo wasiostahili msaada huo waliotafuta kufaidika binafsi. Kwa hiyo Paulo anaweka masharti ili uwezo wa kanisa utumike kwa walio wajane kwelikweli. Kwa wajane vijana njia nzuri si kuandikwa katika jumuiya ya wajane, bali kuolewa.Kama wewe ni mjane, tulia miguuni pake Mungu kwa maombi ili uyatafute mapenzi yake. Mungu akitaka uolewe atakupa mume mwema. Usikate tamaa, uko na Mungu, mume wa wajane.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz