Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Maisha ya ibada yanadai uadilifu na uchaji kwa Mungu. Kwa hiyo tunatakiwa kumaliza mambo kama hasira na kubishana kabla ya kuingia ibadani.Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano(m.8). Watu wanaweza kuvaa mavazi ya thamani ibadani, lakini mioyo yao iko mbali na Mungu. Ibada yao haina maana. Kujipamba kusiwe kwa nje tu kama vile kwa kusuka nywele, kwa dhahabu na lulu, na kwa nguo za thamani, bali kutokane na uchaji ndani ya waabuduo unaofungamana namatendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.(m.10b). Ni wazi kwamba wanaume nao wanahusika vilevile na kujipamba kwa matendo mema. Kiini cha ibada ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli, lakini maisha ya adabu na matendo mema ni ibada vilevile, kwa sababu ibada ya kweli inahusu maisha yetu yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz