Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Umemwombea nani asubuhi hii ya leo? Neno la Mungu linatuambia kuwaombeawatuwote. Paulo anataja kipekee wenye mamlaka ya kisiasa na kiroho, kwa sababu uongozi wao una maana sana kwa amani ya nchi.Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu(m.1-2). Mungu anaongea nasi kwa njia ya Neno lake na sakramenti, wakati sisi tunaongea naye kwa njia ya maombi. Kuomba ni tabia ya kudumu ya maisha ya Mkristo. Ni kumpa Mungu nafasi maishani mwetu.[Mungu] hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli(m.4). Tufanye neno hili kuwa ombi letu kuu kukiwaambea watu wote waokolewe. Mungu ametuahidi kuwa atajibu maombi yetu kila tuombapo:Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa(Mt 7:7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz