Soma Biblia Kila Siku 08/2024Mfano
Paulo anamtia moyo Timotheo. Anamwita “mwanangu”, yaani mwana wake wa kiroho. Anamkumbusha unabii uliotolewa katika mwanzo wa huduma yake, ili kwa kuzingatia ahadi hii ya Mungu, Timotheo aimarishwe kiimani na kupata ujasiri mpya. Tokeo lake lingine ni dhamiri njema. Usipotafuta kujengwa hivyo na neno la Mungu, kwanza utakosa dhamiri safi, kisha imani yako itakufa. Utafanana na Himenayo na Iskanda ambao sio wana wa Mungu tena. Ndivyo Paulo anavyomshauri Timotheo katika 2 Tim 3:14-17. Uyasome maneno yake polepole ukitafakari maana yake:Wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Nane pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Wafalme na 1 Timotheo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz